Na: Tabu Shaibu
Wamiliki wa mashamba, Viwanja na nyumba Kata za Majohe, na Pugu wawasilisha malalamiko kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala
Mhe Sophia Mjema amepokea malalamiko ya Wananchi
waliokuwa na mashamba, viwanja na nyumba katika Kata za Majohe, Pugu, mitaa ya kigilagila, kipunguni na
kinyamwezi kuhusiana na mradi wa upimaji wa viwanja unaotekelezwa na Mamlaka ya
Viwanja vya ndege. Malalamiko hayo yalitolewa katika Mkutano uliofanyika tarehe
4/11/2016 kwenye viwanja vya Ofisi ya Afisa Tarafa ya Ukonga.
Awali wananchi hao
walieleza kuwa, kuanzia mwaka 2001 hadi
2006 Mamlaka ya Viwanja vya Ndege iliendesha zoezi la uthamini wa maeneo
mbalimbali ya wenyeji wa maeneo Majohe, Pugu, Mitaa ya Viwege, Kinyamwezi,
Zavala, Mgeule na Taliani ili kuweza kuwafidia wananchi watakaopisha mradi wa
upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema akipokea malalamiko ya Wananchi wa Pugu na Majohe kuhusu malalamiko ya nyumba na ardhi |