MARUFUKU KUFANYA BIASHARA PEMBEZONI MWA BARABARA ZA MWENDOKASI- DC MJEMA

Na: Hashim Jumbe

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sofia Mjema amepiga marufuku ufanyikaji wa biashara ya aina yoyote pembezoni mwa barabara za mwendokasi, na badala yake maeneo hayo yaachwe kwa matumizi ya watembea kwa miguu.

Agizo hilo limeanza rasmi siku ya leo ya tarehe mosi mwezi Novemba,na kwa Mfanyabiashara yoyote atakayekaidi agizo hilo kuchukuliwa hatua mara moja ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufikishwa Mahakamani.

Bi. Mjema ameyataja maeneo yasiyoruhusiwa kwa upande wa Wilaya ya Ilala kuwa ni maeneo ya Kivukoni front, barabara ya Msimbazi hadi Gerezani, barabara ya Morogoro na maeneo yote yanayopita ma basi ya Mwendokasi.

"Ilala ni kioo cha Jiji la Dar-es-Salaam, maana yake ni kuwa Wageni wanaoingia wote kutoka nje watapita Ilala, hivyo lazima tusimamie sheria na tuhakikishe Ilala inakuwa safi muda wote, maeneo haya ya smart area tusiyaruhusu kufanyika biashara za kiholela holela, maana hizo biashara zinaleta usumbufu sio tu kwa watembea kwa miguu, bali hata kuongeza uchafu maeneo ya Mjini'- DC Mjema
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sofia Mjema akitoa agizo la kukataza ufanyikaji wa biashara pembezoni mwa barabara za Mwendokasi

Kituo cha Posta cha mabasi yaendayo kasi kama inavyoonekana abiria wakipita kwenye maeneo ya watembea kwa miguu, maeneo hayo kwa sasa yamevamiwa na Wafanyabiashara ndogondogo

Barabara ya Msimbazi inavyoonekana kwa sasa baada ya Wafanyabiashara ndogondogo kuvamia maeneo ya watembea kwa miguu


Eneo la mbele la karibia na ofisi za Utumishi ni miongoni mwa maeneo yaliyoathirika na biashara ndogondogo, mbali na kuwa ni kero kwa Watembea kwa miguu lakini pia pamekuwa na uchafu mkubwa unaoachwa na Wafanyabiashara


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi