Na David Langa
Kamati ya Bunge Hesabu za serikali za mitaa LAAC inayoongozwa
na Mh. Rajab Mbarouk (MB) imetembelea
Manispaa ya Ilala na kukagua mapato na matumizi kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 ambapo pamoja na mambo mengine
walitembelea miradi mbalimbali iliyotekelezwa kwa kipindi hicho.
Akitoa ufafanuzi juu ya hali halisi ya Manispaa kwa kipindi
hicho, Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa alisema kwa kipindi hicho Manispaa
imeweza kukusanya zaidi ya shilingio Bilioni 25 na kutekeleza miradi mbalimbali
ikiwemo ujenzi wa madarasa, barabara, vyoo vya wanafunzi, ujenzi wa zahanati
pamoja na ununuzi wa madawati zaidi ya 13,000 kwa shule za msingi.
Kwa upande wake Mgurugenzi wa Manispaa Ndg Isaya Mngurumi
amesema Manispaa imepanga kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii pamoja na kutenga
shilingi milioni 700 kwa ajili ya mfuko wa vijana na akina mama itakayotolewa
kama mkopo kwa wananchi kupitia benki ya wananchi wa Dar es salaa (DCB)
 |
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam Mh. Mecky Sadick akimkaribisha mwenyekiti wa kamati ya Bunge Hesabu za serikali za mitaa Mh. Rajabu Mbarouk na kamati yake katika ukumbi wa mikutano ya Anatoglou . |
 |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Isaya Mngurumi akijibu baadhi ya hoja zilizojitokeza katika mjadala kati yaa kamati ya Bunge na kamati ya fedha na utawala wa manispaa ya Ilala. kushoto kwake ni Mstahiki meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa. |
 |
mwenyekiti wa Kamtri ya Bunge Hesabu za serikali za Mitaa Mh. Rajabu Mbarouk akiongea katika mkutano huo ndani ya ukumbi wa Anatoglou Ilala jiji Dar es salaam |
 |
kamati ya Bunge walipotembelea ujenzi wa ofisi ya kata ya Kivule iliyojengwa kwa fedha za ndani |
 |
mtendaji wa kata ya Kivule akitoa maelezo kwa kamati kwa kamati juu ya ujenzi wa ofisi hiyo iliyogarimu zaidi ya milioni 100,. |
 |
ANkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Isaya Mngurumi akiwatembeza wajumbe wa kamati ya Bunge LAAC kukagua ofisi ya kata ya Kivule |

 |
Mkuu wa Wilaya ya ilala (kulia) akiwaongoza kamati ya Bunge walipotembelea sokpo la samaki Ferry ambalo ni moja ya miradi ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. |
 |
wajumbe ndani ya soko la Ferry . |
 |
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akiongea na vijana wafanyabiashara wa samaki wa soko la Ferry. |