Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala anawatangazia Wakazi pamoja na Wamiliki
wote wa majengo katika Manispaa ya Ilala kuwa, siku ya mwisho ya kulipia kodi
ya majengo kwa mwaka wa fedha wa 2014/15 ni tarehe 30 Juni, 2015. Wote ambao hawajalipia majengo yao wahakikishe
kuwa wanalipa kabla ya tarehe ya mwisho. Wafanyabishara wahakikishe wamelipia
Leseni zao na Ushuru wa Huduma za Jiji. Wote watakaochelewa kulipa watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni
pamoja na kutozwa faini ya asilimia 25 ya kodi anayastahili kulipa.
Lipa
kodi kwa wakati kuepuka usumbufu.
Limetolewa na,
ISAYA M. MNGURUMI
MKURUGENZI
WA MANISPAA,
HALMASHAURI
YA MANISPAA YA ILALA