NAIBU WAZIRI TAMISEMI AFUATILIA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO SOKO LA SAMAKI FERI

Na: Hasim Jumbe


Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo leo ametembelea tena soko la Samaki Feri kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa sokoni hapo mwezi mmoja uliopita.

Awali Mhe. Jafo alitembelea sokoni hapo tarehe 15 Machi, 2016 na kuagiza mambo makubwa matatu yafanyike ndani ya mwezi mmoja.

Maagizo hayo ni, uundwaji wa bodi ya soko la samaki feri, matumizi ya majiko ya kisasa yanayotumia nishati ya gesi yanayolenga kuondosha moshi sokoni hapo na mwisho ni kurekebisha mfumo wa maji machafu sokoni hapo.

Akitoa maelezo mbele ya Mhe. Jafo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Bw. Isaya Mngurumi alieleza kuwa maagizo yote aliyoyatoa Naibu Waziri yalishafanyiwa kazi, ikiwa ni pamoja na uundwaji wa bodi ya soko la samaki feri, marekebisho ya mfumo wa utumiaji wa majiko ya gesi ambapo majiko 48 teyari yamekwishawekwa sokoni hapo na majiko 38 yameshaanza kutumika kwa kukaangia samaki, na mwisho sokoni hapo mfumo wa maji machafu nao umerekebishwa.

Baada ya kupata maelezo ya Mkurugenzi, Mhe. Jafo alifanya ukaguzi sokoni hapo na kupongeza jitihada zilizofanyika
Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo wa kwanza kushoto akimuulizia Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala utekelezaji wa maagizo matatu akiyoyatoa sokoni hapo mwezi mmoja uliopita


Naibu Waziri Jafo akikagua majiko yanayotumia nishati ya gesi soko la samaki feri


Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo akikagua mitungi ya gesi iliyowekwa soko la samaki feri




Kaimu Muhandisi wa Manispaa ya Ilala, Eng. Japhary Bwigane mwenye shati la orenji akimuonesha Mhe. Jafo namna walivyoboresha mfumo wa utiririshaji wa maji machafu sokoni hapo 




Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi