WILAYA YA ILALA YAUKIMBIZA MWENGE WA UHURU NA KUUKABIDHI WILAYA YA TEMEKE

Na: Hashim Jumbe
Tarehe 17 Mei, 2016 Mwenge wa Uhuru ulipokelewa Wilaya ya Ilala kutoka Wilaya ya Kinondoni na kukimbizwa kwenye miradi saba (7) ya kimaendeleo iliyopo Wilaya ya Ilala, miradi hiyo ya sekta ya elimu, afya, mazingira, uvuvi na vikundi vya Ujasiriamali iligharimu jumla ya Shilingi Bilioni 13.7, kati ya miradi hiyo, miradi mitatu ina thamani ya Shilingi Bilioni 10.2 imezinduliwa, miradi miwili yenye thamani ya Shilingi Milioni 805 imewekewa mawe ya msingi na miradi miwili yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6 imekaguliwa na Mwenge wa Uhuru.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond Mushi aliyepo kulia, akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Ally Salum Hapi
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, Bw. George Jakson Mbijima akipata maelekezo alipotembelea moja wapo ya wodi ya Wagonjwa kwenye jengo jipya la hospitali ya Regence 
Bajaji mpya tano(5) za Idara ya Mazingira Manispaa ya Ilala kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa matangazo ya usafi na mazingira kwa Wakazi wa Manispaa ya Ilala, zikiwa teyari kuzinduliwa kwenye mbio za Mwenge


Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, Bw. George Jakson Mbijima akikata utepe kuashiria uzinduzi wa bajaji mpya tano(5) zitakazotumika kuhamasisha usafi kwa Wakazi wa Manispaa ya Ilala



Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, Bw. George Jakson Mbijima akizindua Zahanati ya Yongwe iliyopo Chanika




Kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka 2016 akiangalia namna ya utotoreshaji wa samaki kwenye bwawa la samaki Kinyamwezi-Pugu

Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, Bw. George Jakson Mbijima akiweka jiwe la msingi ujenzi wa madarasa shule ya msingi Maghorofani



Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Sophia Mjema aliyepo kulia, akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi