Na: Hashim Jumbe
Shule za Msingi za Manispaa ya Ilala, zimeendelea kunufaika na misaada mbalimbali kutoka kwa Wadau wanaounga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano, kwa kusaidia kufanikisha upatikanaji wa nyenzo muhimu za mahala pa kujifunzia ikiwemo upatikanaji wa madarasa na madawati.
Awali, Benki ya Diamond Trust ilifanikisha upatikanaji wa vyumba viwili vya madarasa vyenye thamani ya Shilingi milioni 30 kwa shule ya Msingi Jitihada iliyopo Kata ya Kitunda, na sasa wamekamilisha upatikanaji wa madawati 200 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa shule hiyo, hivyo kufikisha mchango wa shilingi milioni 50.
Madawati hayo yalipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sofia Mjema aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa.