Na
David Langa.
Mpango
wa kunusuru Kaya masikini (TASAF) wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala umetoa
jumla ya shilingi milioni 292 kwa ajili ya kusaidia kaya masikini 6115 za wilaya
hiyo.
Fedha
hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Saalam na Mratibu wa TASAF wa Halmashauri
hiyo, Mwaluma Msofe ambaye amesema kuwa fedha hizo zitagawanywa kwenye mitaa 74
ya Halmashauri hiyo kwa kuwa ndiyo walengwa wa mpango huo.
Msofe
ameongeza kuwa mchakato wa kuwapata wananchi wenye maisha magumu unafanywa na
wananchi wenyewe katika mtaa husika ambapo baada ya kuwatambua wanathibitishwa mbele ya mkutano wa mtaa.
“Fedha
tunazowapatia wananchi hawa zimeanza kuonyesha mafanikio kwa kuwa zimesaidia
kaya hizo kuanzisha miradi midogo midogo inayowawezesha kuendeleza maisha yao
pia fedha hizo zimesaidia watoto kupata mahitaji muhimu ya shule hivyo
kupelekea mahudhurio kuongezeka”, alisema Msofe
Mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Ilala, Mwaluma Msofe |
Mratibu
huyo amefafanua kuwa kuna aina mbili za ruzuku ambazo ni ruzuku ya msingi
ambayo kaya masikini hupewa kwa mtu yeyote anayetambuliwa na mpango huo wakati
ruzuku ya masharti hutegemea na aina ya familia.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimanga- Darajani, Chacha Mwenge
amesema kuwa anaendelea na kazi ya kusimamia na kuchambua majina ya wahusika
kwa kuwa kuna baadhi ya wananchi waliingizwa katika mpango huo bila kuwa na
sifa kutokana na wananchi hao kutoa taarifa za uongo wakati wa utambuzi.
“Tumegundua
kuwa kuna baadhi ya kaya ambazo
zimeingia kwenye mpango huu kimakosa kwahiyo tunaendelea kuzitoa, hadi
sasa jumla ya kaya 28 za mtaa wetu tumeshaziondoa kwa sababu ya kukosa sifa”,
alisema Mwenge.
Baadhi ya wanufaika na Mradi wa TASAF wakisubiri majina yao kuhakikiwa kata Mtaa wa Kimanga-Darajani kata ya Kimanga,Manispaa ya Ilala |
Naye
mmoja wa wananchi wanaonufaika na mpango huo, Ayubu Kabeta ameishukuru Serikali
kwa kuwapatia fedha za kujikimu pia ameiomba kuongeza kiwango cha fedha hizo
kwa kuwa kiasi ni kidogo bado hakikidhi huduma muhimu.