Na: Hashim Jumbe
Kamati ya Fedha na Utawala Manispaa ya Ilala, imeanza ziara ya siku mbili kukagua miradi ya kimaendeleo inayoendelea katika sehemu mbalimbali za Manispaa hiyo. Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, kamati imetembelea matengenezo ya barabara ya Mombasa-Moshibar, Ujenzi wa madarasa 21 shule ya msingi Maghorofani, Ujenzi wa madarasa 6 shule ya sekondari Juhudi na Ujenzi wa mfumo wa mtandao wa maji na mtandao wa mabomba ya maji Pugu-Bangulo.
Hali ya Miradi iliyotembelewa hadi hivi sasa:
4. Ujenzi wa mfumo wa mtandao wa maji na mtandao wa mabomba ya maji Pugu-Bangulo: Mkandarasi ni M/S Gwantwa Contractors Ltd, mradi unajengwa kwa fedha za Halmashauri na ulikamilika tangu Julai 2015, mradi umetumia jumla ya fedha Milioni 83.7, hali ya mradi ni umekamilika uko kwenye majaribio na marekebisho sehemu zitakazokuwa na hitilafu
Kamati ya Fedha na Utawala Manispaa ya Ilala, imeanza ziara ya siku mbili kukagua miradi ya kimaendeleo inayoendelea katika sehemu mbalimbali za Manispaa hiyo. Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, kamati imetembelea matengenezo ya barabara ya Mombasa-Moshibar, Ujenzi wa madarasa 21 shule ya msingi Maghorofani, Ujenzi wa madarasa 6 shule ya sekondari Juhudi na Ujenzi wa mfumo wa mtandao wa maji na mtandao wa mabomba ya maji Pugu-Bangulo.
Hali ya Miradi iliyotembelewa hadi hivi sasa:
- Matengenezo ya barabara ya Mombasa-Moshibar: mradi huu wa matengenezo ya barabara kwa kiwango cha lami ni wa kilomita 1.65 unasimamiwa na Mkandarasi anayeitwa 'Delmonte (T) Ltd, umeanza mwezi February 2016 na unatarajia kukamilika mwezi February 2017, mradi unafadhiliwa na fedha ya mfuko wa barabara, fedha iliyokisiwa kutumika ni bilioni 2.45. Hadi sasa kazi ya kuweka box calvat 3 zimekamilika, na kazi ya kuweka tabaka la pili la changarawe inaendelea
2.Ujenzi wa madarasa 6 shule ya sekondari Juhudi: Mkandarasi ni 'Ibrahim Hamis Kuwilu' ujenzi umeanza mwezi February 2016 na ulitarajiwa kukamilika Juni 2016, hali ya mradi ni madarasa manne yamekamilika na yanatumika na mawili yapo katika hatua za mwisho za umaliziaji, fedha inayotumika ni ya Halmashauri, jumla ya shilingi Milioni Mia Moja na Thelathini na Mbili.
3. Ujenzi wa madarasa 21 shule ya msingi Maghorofani: Mkandarasi ni 'Wajenzi Enterprises', mradi umeanza Machi 2016 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Septemba 2016, hali ya mradi hadi sasa jumla ya vyumba 16 vya madarasa , ofisi moja na matundu 10 vimekamilika kwa fedha toka Serikali Kuu iliyokisiwa kuwa Milioni Mia Mbili na mbili na fedha kiasi cha Shilingi Milioni Mia Moja na Sabini na Sita ndizo zimetumika.Aidha ujenzi wa madarasa matatu yamekamilika na mengine matatu yako katika hatua ya msingi, fedha ni kutoka Halmashauri na ni kiasi cha Milioni Themanini na Tano.