Na: Hashim Jumbe
Ziara ya Kamati ya Fedha na Utawala Manispaa ya
Ilala imeendelea kwa siku ya pili kwa kutembelea miradi mingine sita
inayondelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Ilala, katika
siku ya pili ya ziara hiyo Kamati ya Fedha na Utawala imetembelea; Ujenzi wa
Hospitali mpya ya Chanika, Ujenzi wa Zahanati ya Lubakaya, Ujenzi wa Zahanati
ya Luhanga,Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya-Kivule, Ujenzi wa vyumba vya madarasa
13 Kimwani Mpya na Ujenzi wa madarasa manne shule ya Sekondari Kitunda.
Hali
ya Miradi hadi hivi sasa:
1. Ujenzi
wa Hospitali mpya ya Chanika:
Mradi
huu unasimamiwa na Mkandarasi anayeitwa ‘China Hunan Engineering Construction
Group(EA)’ambao umeanza tarehe 19 Januari, 2016 na unatarajiwwa kukamilika
tarehe 1 Januari, 2017, mradi huu unafadhiliwa na Serikali ya Korea Kusini
(KOICA) na fedha zilizoidhinishwa ni USD 1,799,789, Hali ya mradi ni jengo la
hospitali limefikia kwenye linta na jengo la makazi ya Wafanyakazi limefikia
hatua ya kupauliwa.
2. Ujenzi
wa vyumba vya madarasa 13 Kimwani Mpya:
Mradi
huu unasimamiwa na Mkandarasi anayeitwa ‘Kijiji Trans Co. Ltd’, umeanza mwezi
Machi 2016 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Semptemba, 2016, fedha za ujenzi
wa mradi huu ni kutoka Serikali Kuu iliyotoa Kiasi cha Shilingi Milioni Mia
Moja na Sabini kwa ujenzi wa vyumba 10 ambavyo teyari vimeshakamilika, na fedha
nyengine ni za Halmashauri nazo ni Jumla ya Shilingi Milioni Hamsini na Moja
ambazo zenyewe ziemjenga madarasa matatu ambapo hadi sasa ujenzi wa vyumba vya
madarasa mawili viko katika hatua ya linta na ujenzi wa darasa moja uko katika
hatua ya msingi.
3. Ujenzi
wa Zahanati ya Lubakaya:
Ujenzi
unasimamiwa na Mkandarasi anayeitwa ‘Gwantwa Construction’ na ulianza tarehe 25
Disemba, 2016, mradi unatekelezwa kwa fedha za Halmashauri zipatazo Milioni
64.7 na hadi sasa ulipofikia ni kwenye ujenzi wa msingi, kuinua kuta hadi hatua
ya boma.
4. Ujenzi
wa Zahanati ya Luhanga:
Ujenzi
unasimamiwa na Mkandarasi ambaye ni ‘Suma JKT’ na ulianza Julai, 2013 na
ulitarajiwa kukamilika Agosti, 2015 mradi ulitengewa jumla ya fedha Milioni 70
na hadi sasa zimetumika Milioni 60. Hali ya utekelezaji iliyofikiwa ni ujenzi
wa msingi, ujenzi wa kuta hadi hatua ya upanuaji, upanuaji mbao za ceiling
board
5. Ujenzi
wa Hospitali ya Wilaya-Kivule:
Mradi
unasimamiwa na Mkandarasi ‘Skol Building Contractor’ mradi huu ulianza mwezi
Julai 2015 na ni mradi unaojengwa kwa fedha za Halmashauri ambazo ni makisio ya
Shilingi Bilioni 1.019. Hadi sasa mradi huu umefikia kwenye ujenzi wa msingi wa
ghorofa mbili na uinuaji nguzo 78 za ghorofa mbili
6. Ujenzi
wa madarasa manne shule ya Sekondari Kitunda:
Mkandarasi
anayesimamia ujenzi anaitwa ‘William Masaba’ na mradi huu umeanza mwezi Machi,
2016 na ulikamilika mwezi Mei, 2016, fedha zilizotumika ni za Halmashauri na ni jumla ya Shilingi Milioni 88