KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA MANISPAA YA ILALA YAMALIZA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI KWA MAFANIKIO MAKUBWA

Na: Hashim Jumbe
Ziara ya kukagua Miradi ya maendeleo kwa Manispaa ya Ilala imemalizika huku ziara hiyo ikionekana kuwa na tija kwa miradi inayoendelea kutekelezwa kwenye Manispaa hiyo, ambapo kupitia ziara hiyo Kamati ya Fedha na Utawala wameweza kubaidi baadhi ya mapungufu na kuyatolea ufafanuzi. Miradi minginge tisa ilitembelewa na Kamati hiyo na hali ya miradi hiyo ni kama ifuatayo:

1. Ujenzi wa upanuzi wa jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) Hospitali ya Amana awamu ya kwanza:
Ujenzi unasimamiwa na Mkandarasi anayeitwa 'Meph Investment' na ulianza tangu tarehe 2 Mei, 2013 na ulitarajiwa kukamilika tangu Disemba 2013, hali ya mradi hadi hivi sasa ni kumejengwa nguzo 18, msingi, uwekaji wa zege na sakafu, fedha zilizokisiwa kwenye ujenzi ni Shilingi Milioni 231,680,000/= mradi unajengwa kwa fedha za Halmashauri, kwa sasa ujenzi umesimama unasubiri mkataba wa awamu ya pili.



2. Ukarabati wa machinjio ya Vingunguti:
Ukarabati huu umesimamiwa na ‘Local Fundi’ na ulianza mwezi wa Februari 2016 na umekamilika Julai 2016, ambapo ukarabati huo umehusu ujenzi wa sehemu maalumu ya kutumbulia matumbo ya Wanyama waliochinjwa uliogharimu fedha kiasi cha shilingi Milioni 9.7, ujenzi wa reli za chuma maalumu sehemu ya kuchunia mbuzi, gharama zake ni shilingi Milioni 5.6, ujenzi wa paa na kuezeka mabati eneo la kuoshea utumbo, gharama zake ni shilingi Milioni 1.5, ukarabati eneo la kushushia n’gombe, kujaza mawe kwenye mashimo katika eneo hilo, kuongeza culvert na kujenga eneo nje ya geti la kuingizia n’gombe, gharama zake ni jumla ya fedha milioni 10.5, ujenzi wa ukuta kutenganisha eneo la kuchinjia na kusubirishia nyama, shimo la kutupia mizoga,kuweka zege, kuweka marumaru na kupaka rangi jengo la kuchinjia, ujenzi na ukarabati wa mferji wa maji taka na ujenzi wa kibanda cha walizi, gharama zilizotumika ni Milioni 84.7









3. Ujenzi wa barabara ya Vingunguti-Barakuda:
Ujenzi ni wa kiwango cha lami na urefu ni kilomita 1.34, Mkandarasi ni ‘Patty Enterprise’, hali ya mradi hadi hivi sasa ni barabara imewekwa tabaka la udongo na saruji awamu ya kwanza, fedha ni za mfuko wa barabara ‘road fund’ na zilizotumika ni Milioni 694



4. Ujenzi wa barabara ya St. Mary’s:
Ujenzi ni wa kiwango cha lami na urefu ni kilomita 1.2, Mkandarasi ni ‘Delmonte (T) Ltd’, hali ya mradi hadi hivi sasa ilipofikia ni kwenye uchimbaji wa sehemu korofi ya barabara, kupanga mawe, ujenzi wa mfereji wa nyongeza na kumwaga zege kwenye eneo korofi mita 245, fedha zinazojengea ni za Halmashauri, na zilizotengwa ni Milioni 532


5. Ujenzi wa barabara ya Kimanga-Mazda:
Ujenzi ni wa kiwango cha lami na urefu ni kilomita 0.8, Mkandarasi ni ‘Delmonte (T) Ltd’, mradi umeanza mwezi Machi,2016 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2017, hali ya mradi hadi hivi ipo kwenye kusaga tabaka la lami, kusambaza na kushindilia, kuchimba mifereji kwa ajili ya service ducts shughuli hizi zimekamilika, kazi inasubiri usanifu wa mwisho, fedha zinazojengea ni za Halmashauri, na zilizotengwa ni Milioni 915.


6. Ujenzi wa barabara ya Kilomita 2 na daraja la chuma barabara ya Kinyerezi-Bonyokwa:
Mkandarasi ni 'M/S Texas Construction', ujenzi ulianza mwezi Machi 2015 na unatarajiwa kuisha mwezi Septemba 2016, fedha zinazojengea ni za Mfuko wa Barabara  ambazo ni Milioni 330.7



7. Ujenzi wa matundu 24 ya vyoo vya Wanafunzi Kinyerezi Sekondari:
Mkandarasi ni 'Kinara S. Kinara', ujenzi ulianza mwezi Julai  2015 na ulitarajiwa kuisha mwezi Juni 2016, fedha zinazojengea ni za Halmashauri  ambazo ni Milioni 48





8. Ujenzi wa vyumba vya madarasa 6 shule ya msingi Kinyerezi JAICA:
Mjenzi ni ‘Nali Engineering Works Contractors Ltd’, ujenzi umeanza mwezi Julai 2016 na unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba 2016, fedha za ujenzi ni za Halmashauri na makisio yake ni Milioni 102





9. Ujenzi wa box kalavati barabara ya Saranga-Kinyerezi:
Mkandarasi ni ‘M/S Mavonda Co. Ltd’, ujenzi umeanza mwezi Februari 2015 na unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2016, jumla ya fedha zilizokisiwa kwenye ujenzi ni milioni 385.4 na fedha ni za mfuko wa barabara.






Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi