Na:
Hashim Jumbe
Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Manispaa ya Ilala
imetembelea Shule zenye mahitaji maalum za Uhuru Mchanganyiko na Buguruni
Viziwi ambapo kamati hiyo imejionea changamoto mbalimbali shuleni hapo ikiwa ni pamoja na ubovu wa vyoo na mahitaji mengine ya vifaa vya kujifunzia.
Kamati hiyo ilifanya pia ziara kwenye Zahanati ya Kitunda na kupokea changamoto za utoaji huduma kwenye Zahanati hiyo zinazosababishwa na idadi kubwa ya Wagonjwa wanaofika kwenye Zahanati hiyo kutokea kwenye Kata za jirani ikiwa ni pamoja na Kata ya Mzinga na Kitunda. Kutokana na changamoto hizo Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo ameiomba Kamati waangalie uwezekana wa kuipandisha hadhi Zahanati hiyo na kuwa Kituo cha Kutolea Huduma.