MSTAHIKI MEYA ILALA AZINDUA MADARASA MATANO SHULE YA MSINGI BONYOKWA NA KUWAPONGEZA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI MTIHANI WA DARASA LA SABA

Na: Hashim Jumbe
Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala, Mhe. Charles Kuyeko, leo amezindua vyumba vya madarasa matano ya shule ya Msingi Bonyokwa yaliyojengwa kwa fedha kiasi cha Shilingi Milioni 80 kutoka kwenye Mfuko wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, ikiwa ni moja ya mipango ya kuhakikisha Wanafunzi wa shule zote za Manispaa ya Ilala wanapata elimu katika mazingira yaliyoboreshwa.

Ujenzi wa madarasa hayo umezingatia ongezeko la uandikishaji wa Wanafunzi katika shule hiyo uliochagizwa na sera ya elimu bila malipo kama ilivyoelekezwa kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 inayoelekeza kufuta karo za shule na michango mingineyo, hivyo kupelekea kuwepo idadi kubwa ya uandikishaji wa Wanafunzi.

Aidha, katika uzinduzi huo, Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala, Mh. Charles Kuyeko aliwapongeza Wanafunzi wanne waliomaliza darasa la Saba mwaka huu wa 2016 shuleni hapo na kupata Ufaulu wa daraja 'A', Wanafunzi hao ni Frank Julias Francis, Gervas Makishe, Joel Mwakyoma na Tarik Kage. Mstahiki Meya ametoa ahadi ya fedha taslimu kiasi cha Shilingi laki moja kwa kila Mwanafunzi.



Kaimu Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Ndugu Hamis Mlangala akifanya utambulisho wa Wageni kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Manispaa ya Ilala


Mkuu wa Shule ya Msingi Bonyokwa akimkabidhi risala Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe. Charles Kuyeko

Wazazi na Walenzi wa Wanafunzi wa shule ya msingi Bonyokwa walipohudhuria kwenye sherehe ya uzinduzi wa vyumba vya madarasa shuleni Bonyokwa



Mstahiki Meya Ilala, Mhe. Charles Kuyeko akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2016


Mstahiki Meya Ilala, Mhe. Charles Kuyeko akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa vyumba vitano vya madarasa shuleni Bonyokwa




Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi