Na: Hashim Jumbe
Kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kimepokea taarifa ya utendaji kazi wa Kamati
za Kudumu za Halmashauri kwa kipindi cha Julai hadi Septemba, 2016, taarifa nyengine
iliyopokelwa na kupitishwa ni maombi ya kufanya marekebisho ya jedwali la tozo
za machinjio katika Sheria Ndogo ya Biashara ya zao la ngozi na ada za
machinjio za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Taarifa ya awali kuwasilishwa ilikuwa ni taarifa utendaji
kazi ya Kamati ya Fedha na Utawala iliyowasilishwa na Naibu Meya kwa niaba ya
Mwenyekiti wake ambaye ni Mstahiki Meya, akiwasilisha taarifa hiyo, Naibu Meya
Mhe. Omary Kumbilamoto alisema “katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi
Septemba, 2016 Kamati ya Kudumu ya Fedha na Utawala imesimamia utekelezaji wa shughuli
mbalimbali za uendeshaji wa miradi ya maendeleo kupitia vikao vyake vya
kikanuni”
Aidha, Kamati hiyo kwa kipindi hicho cha Julai hadi
Septemba ilijiwekea lengo la kukusanya mapato ya Shilingi Bilioni 19.9 ambapo
zimekusanywa Shilingi Bilioni 11.3 sawa na asilimia 57 ya lengo la robo ya
kwanza ya mwaka.
Kamati nyengine iliyowasilisha taarifa yake ni
Kamati ya Mipangomijinna Mazingira na Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii.
Taarifa zote zilipokelewa na kujadiliwa na Wajumbe kisha
zikapitishwa ikiwa ni pamoja na taarifa ya kufanyiwa marekebisho ya jedwali la
tozo za machinjio iliyowasilishwa na Mkuu wa Idara ya Uvuvi na Ufugaji Bw.
Msongo Songoro