DC-MJEMA ARUDI KUKAGUA UKARABATI WA SHULE ILIYOHARIBIWA NA UPEPO

Na: Hashim Jumbe
Miongoni mwa athari zilizosababishwa na upepo mkali ulioambatana na mvua zilizonyesha Jumatatu ya tarehe 06 Machi, 2017 kwenye maeneo ya Kata za pembezoni mwa Manispaa ya Ilala ni kuharibika vibaya kwa madarasa matatu, ofisi ya Walimu na miundombinu mingine kwenye shule ya msingi Kigogo Fresh, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe, Sophia Mjema alitembelea shuleni hapo na kujionea athari hizo na kisha kutoa agizo la ukarabati wa haraka kwa jengo hilo.

Tarehe 29 Machi, 2017 Mhe. Mjema ametembelea shuleni hapo na kujionea ukarabati uliofanyika wa jengo hilo uliotumia jumla ya shilingi Milioni 42.

"kutokana na maagizo niliyoyatoa, natumaini hadi kufikia Ijumaa madarasa yatakuwa yamekamilika na siku ya Jumatatu wale Wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili tuliowapumzisha nyumbani kupisha ukarabati huu wataanza kuyatumia madarasa" alisema Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Mjema
Jengo la shule ya msingi Kigogo Fresh lililoathiriwa na upepo mkali na mvua iliyonyesha tarehe 6 Machi,2017 lilivyokuwa linaonekana kabla ya kufanyiwa ukarabati

Muonekano wa sasa wa jengo la madarasa na ofisi iliyoathiriwa na upepo na mvua shuleni Kigogo Fresh baada ya kufanyiwa ukarabati




Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema akizungumza na Walimu shuleni hapo mara baada ya kufanya ukaguzi wa jengo la madarasa na ofisi
Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Mjema aliitembelea familia iliyompoteza Mama yao kufuatia kuangukiwa na mti mkubwa uliosababishwa na mvua na upepo iliyonyesha siku ya Jumatatu maeneo ya Majohe-Bombambili





Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi