Na: Hashim Jumbe
Jumamosi ya pili ya kila mwezi ni siku ambayo Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe. Dr. John Joseph Magufuli imeagiza Wananchi wake wote kushiriki kwenye zoezi la usafi kuanzia kwenye maeneo wanayoishi hadi kwenye maeneo wanayofanyia biashara.
Zoezi hilo kwa Mkoa wa Dar-es-Salaam linaanza saa 12:00 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi ambapo Wananchi hujitokeza kufanya usafi huku wakipata hamasa kutoka kwa Viongozi wao kuanzia ngazi ya Mtaa,Kata na hatimaye Viongozi wa Wilaya na Halmashauri.
Kwa upande wa Manispaa ya Ilala, zoezi la usafi limekuwa likitekelezwa na kusimamiwa na Kata husika huku Wakuu wa Idara kutoka Halmashauri wakiwa Walezi wa Kata hizo, hivyo wanakuwa na wajibu wa kusimamia usafi wa Kata husika.
Mbali na hilo, Manispaa ya Ilala ina timu inayosimamia usafi ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya, ambapo kazi kubwa ya timu hiyo ni kuhamasisha usafi kwa kushiriki usafi katika maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo.
Katika kushiriki kwenye zoezi la usafi wa Jumamosi ya mwisho wa mwezi Aprili, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema amebadili mbinu za kushiriki usafi kwa kukagua magari yanayobeba abiria kama yana vyombo vya kubebea uchafu na kuyatoza faini magari yasiyokuwa na vifaa vya kubebea taka.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Ilala pamoja na Wataalamu wa Manispaa ya Ilala, wametumia siku ya leo kuwaelimisha Madereva wa bajaji namna ya kutunza mazingira huku wakiwaagiza kutafuta vyombo vya kubebea taka kwenye bajaji zao.
Lakini, katika hali nyengine Mkuu wa Wilaya ya Ilala amewapiga marufuku Wafanyabiashara wanaopanga bidhaa zao chini maeneo ya kituo cha mabasi ya UDART Kivukoni