MKURUGENZI MANISPAA YA ILALA ASHIRIKI FUTARI NA WANAFUNZI WENYE UHITAJI MAALUM, NAIBU MEYA ATOA AHADI YA MBUZI

Na: Hashim Jumbe
Ramadhani ya 13, Naibu Meya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, pamoja na Watendaji wengine kutoka Idara ya Elimu Msingi na Idara ya Fedha Manispaa ya Ilala, wameitumia kujumuika kwenye futari na Wanafunzi wanye mahitaji maalum kutoka shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko na Shule ya Viziwi ya Buguruni.

Futari hiyo iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, ilikuwa na lengo la kuimarisha ukaribu kati ya Wanafunzi, Walimu, Walezi pamoja na Viongozi wenye dhamana na Wanafunzi hao.

Akiongea wakati wa futari hiyo, Naibu Meya Manispaa ya Ilala, Mhe. Omary Kumbilamoto alisema "Binafsi nilikuwa sijui kuwa Wanafunzi hawa wa kwetu wana uhitaji mkubwa wa huduma pamoja na mambo mengine muhimu, siku zote tumekuwa tukitoa misaada kwa Watu wengine, kumbe tuna Watoto wenye uhitaji zaidi, sasa ninawaahidi nitarudi tena kuwatembelea na nitawaletea Mbuzi wawili"

Wanafunzi wenye uhitaji maalum toka shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko na Buguruni Viziwi wakipata futari ya pamoja iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Bw. Msongela Palela akizungumza na Wanafunzi pamoja na Waalikwa wengine waliohudhuria kwenye futari hiyo iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala
Naibu Meya Manispaa ya Ilala, Mhe.Omary Kumbilamoto akizungumza wakati wa hafla ya futari iliyofanyika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko
                                   

1 Maoni

  1. Asante baba kwa kuwakumbuka hawa ndugu zetu wewe umeonesha upendo Mungu atakulipa kwa wema huu. Hongera

    JibuFuta
Mpya zaidi Nzee zaidi