RC-MAKONDA AKABIDHI KWA HALMASHAURI NA MKOA KOMPYUTA 50 ALIZOPOKEA KUTOKA KAMPUNI YA TAMOBA

Na: Hashim Jumbe
Mkuu wa Mkoa wa DSM, Mhe. Paul Makonda leo amekabidhi kompyuta 50 zenye jumla ya thamani ya Shilingi Milioni 85 alizopokea kutoka Kampuni ya Ulinzi ya TAMOBA, ikiwa ni azma yao ya kuunga mkono utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya Tano, chini ya Muheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.

Kompyuta hizo 50 ziligawanywa kwa Manispaa ya Ilala kupata Kompyuta 8, Ubungo 8, Kigamboni 8, Kinondoni 8, Temeke 8, Halmashauri ya Jiji la DSM walipata Kompyuta 5 na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa nao walipata kompyuta 5












Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi