Na: George Mwakyembe
Semina ya kuwajengea uwezo wenyeviti wa
mitaa, watendaji wa mitaa pamoja na watendaji wa kata imefanyika tarehe 19 na 20 mwezi Oktoba
katika ukumbi wa shule ya sekondari Tambaza , Semina hiyo ambayo imeandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam kwa kushirikiana na Halmasahauri ya Manispaa ya Ilala.
Lengo la semina hiyo ni
kuwajengea uwezo watendaji hao ambao ni nguzo muhimu sana iliyo karibu na jamii yetu.
Maada mbali mbali zilitolewa na
wataalamu kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa
pamoja na ofisi ya Uhamiaji. Baadhi ya maada zilizotolewa ni
Uhamiaji haramu , Sheria za mazingira , Ulinzi na usalama
, usimamizi wa ardhi, Taratibu
za fedha katika ngazi ya kata na
mitaa, Utawala bora, usafi wa
mazingira, Pamoja na sheria, sera,
kanuni na miongozo ya maji. Katika maada
zote hizo maada ambayo ilikuwa ni ngeni
na ilipokelewa kwa maswali mengi ni Uhamiaji haramu. Kama unavyojua uhamiaji haramu limekuwa
tatizo katika mkoa wa Dar es salaam wahahamiaji wamekuwa wakiongezeka na kuhamia
bila kufuata utaratibu,
wahamaiji wamekuwa wakitoka nchi za jirani kama Uganda,Kenya,Somalia,Rwanda na nchi nyingine
nyingi .
Washiriki
walifundishwa jinsi gani ya kumtambua mhamiaji haramu na hatua gani anatakiwa
kuchukua pindi anapokuwa amegundua na
kijidhihirisha kuwa huyu si mwenyeji
bali ni mhamiaji, walifundishwa
na namna ya kuwafichichua watu wote wanaowaficha wahamaiaji haramu kwa kujenga mazingira ya kujipatia kipato.