DC-MJEMA AZINDUA JENGO LA WAZAZI ZAHANATI YA MVUTI BAADA YA KUFANYIWA MAREKEBISHO

Na: Hashim Jumbe
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema amefanya uzinduzi wa jengo la Wazazi katika Zahanati ya Mvuti baada ya kufanyiwa marekebisho yaliyogharimu jumla ya Shilingi Milioni 69.5 ambapo Wananchi wa Mtaa wa Mvuti walichangia Shilingi Milioni 20.1 na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilichangia Shilingi Milioni 49.5.

Aidha, Zahanati ya Mvuti iliyoanzishwa mwaka 1976 inahudumu jumla ya Wakazi wapatao 24,461 huku jengo hilo la wodi ya Wazazi lililoanzishwa mwaka 2013 kwa jitihada za Wananchi pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala limeweza kupunguza msongamato na kufanya upatikanaji wa huduma kwa Mama kuwa katika mazingira mazuri
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema akiongoza kwenye ukataji utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa jengo la Wazazi kwenye Zahanati ya Mvuti baada ya kufanyiwa marekebisho
Jengo la akina Mama lililofanyiwa ukarabati kwenye Zahanati ya Mvuti linavyoonekana baada ya ukarabati



Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akikagua wodi ya Wazazi baada ya kufanyiwa ukarabati





Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akiwa na mmoja ya Watoto waliowahi kuzaliwa kwenye Zahanati ya Mvuti 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi