DC MJEMA AWATAHADHARISHA WANANCHI WA WILAYA YA ILALA KUJIEPUSHA NA MAAMBUKIZI YA KIFUA KIKUU

Na: Hashim Jumbe

Tarehe 24 Machi ya kila mwaka ni siku ya kifua kikuu Duniani na kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya kifua kikuu ya mwaka 2017, Tanzania ni miongoni mwa Nchi 30 Duniani zenye kiwango kikubwa cha ugonjwa wa kifua kikuu, ikichukuwa nafasi ya 6 kiulimwengu na nafasi ya 4 kwa Afrika.

Kwa mwaka huu wa 2018 maadhimisho ya Siku ya kifua kikuu Duniani yamebeba ujumbe usemao "Viongozi tuwe Mstari wa mbele kuongoza Mapambano yakutokomeza kifua kikuu" na kwa upande wa  Manispaa ya Ilala wameadhimisha leo siku hiyo ikiwa ni siku moja kabla ya siku ya Kifua kikuu Duniani.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kudhibiti kifua kikuu mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Bibi Victorina Ludovick alisema "Kama unavyofahamu Mkoa wa Dar es Salaam unachangia kwa kiasi kikubwa idadi ya Wagonjwa wa Kifua Kikuu Nchini na Manispaa ya Ilala ikiwa ni miongoni wa eneo la jiji la Dar essalaam. Hii inachangiwa na shughuli nyingi za kiuchumi kufanyika katika Manispaa yetu na hivyo misongamano ya Watu na ,makazi ni mikubwa sana katika Masipaa ya Ilala"

"Kata za Buguruni, Ukonga, Kiwalani, Mchafukoge na Vingunguti ndiyo zenye idadi kubwa ya Wagonjwa wa Kifua Kikuu, kwa wastani Kata hizo huchangia asilimia 80 ya Wagonjwa wote takribani 5,000 wanaogundulika kuwa na Kifua Kikuu kwa mwaka" alimalizia Mkuu Mkuu

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema alitoa tahadhari yakujiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu huku akitoa wito kwa Wagonjwa wenye maambukizi kujitokeza na kupatiwa tiba “Ni matumaini yangu kwamba maaadhimisho haya yatakuwa ni chachu yakuongeza bidii katika mapambano yakutokomeza Kifua Kikuu nchini. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha Wagonjwa wenye kifua kikuu wanaibuliwa na kupatiwa matibabu kwa wakati”









Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi