MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI: DC MJEMA AWEKA JIWE LA MSINGI KWENYE UJENZI WA TANKI LA KUHIFADHIA MAJI KATA YA KISUKURU

Na: Hashim Jumbe

Katika muendelezo wa wiki ya maadhimisho ya maji kwa Wilaya ya Ilala, leo hii Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Sophia Mjema, ameweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lililopo Kata ya Kisukuru Manispaa ya Ilala.

Mradi huo wa ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji, unatekelezwa kwa fedha za makusanyo ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, chini ya usimamizi wa Mhandisi wa Maji wa Halmashauri na Mkandarasi anayetekeleza Mradi huo akiwa ni Kampuni ya Musufini General.

Katika utekelezaji wa Mradi huo, tanki linalojengwa lina uwezo wa kuhifadhi lita za maji zenye ujazo wa lita 150,000 na litaunganishwa na Miundombinu ya DAWASCO kwa ajili ya kutoa huduma kwa Wananchi wa Kata ya Kisukuru., huku gharama zake zikiwa ni Jumla ya Shilingi Milioni 113.4
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ambaye ni Afisa Elimu Msingi wa Manispaa hiyo, Bibi Elizabeth Thomas akifanya utambulisho wa Wageni wakati wa hafla fupi ya uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji Kata ya Kisukuru iliyopo Manispaa ya Ilala.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mhe. Charles B. Kuyeko akisalimiana na Waaalikwa waliohudhuria kwenye hafla hiyo


Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema akikata utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lililopo Kata ya Kisukuru






Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi