Na: Hashim Jumbe
Tupo kwenye wiki ya Maadhimisho ya Maji, iliyobeba Kaulimbiu "Hifadhi Maji na Mifumo ya Kiikolojia kwa Maendeleo ya Jamii" na leo hii Diwani wa Kata ya Ilala, Mhe. Saady Khimji amezindua rasmi Mradi wa Maji ya kisima kirefu kilichochimbwa Mtaa wa Sharifu Shamba, Kata ya Ilala.
Mradi huo umetekelezwa kwa fedha za ndani za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Jumla ya Shilingi Milioni 32.6 umegharamia Mradi, ambapo Mkandarasi aliyetumika ni Kampuni ya Matrix Teknoloji na Mradi umesimamiwa na Mhandisi wa Maji wa Manispaa ya Ilala.
Kukamilika kwa Mradi huo wa Kisima cha Maji chenye ujazo wa lita 13,200 kwa saa unatazamiwa kuhudumia Wananchi wapatao 3,960 kwa wastani wa matumizi ya ndoo tatu za ujazo wa lita 20 kwa kila Mkazi kwa siku.

Diwani wa Kata ya Ilala, Mhe. Saady Khimji akizindua Mradi wa Kisima kirefu cha Maji Mtaa wa Sharifu Shamba |