MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA ILALA AZINDUA JENGO LA OFISI YA MTAA WA MTAKUJA

Na: Hashim Jumbe
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mhe. Charles Kuyeko leo amezindua jengo la Ofisi ya Mtaa wa Mtakuja katika Kata ya Vingunguti, ikiwaa ni ahadi ya Serikali ya kuwapatia Wananchi huduma rafiki kwa maana ya kuhifadhi siri na uhuru wa Wananchi wanapopata huduma huku ikiwa inayotolewa kwenye mazingira yaliyoboreshwa.

Ujenzi wa Ofisi hii ni kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri, hivyo kiasi cha Shilingi Milioni 49.9 zimetumika wakati wa ujenzi huo.

"Kabla ya kujenga Ofisi hii tulikuwa tukitoa huduma kupitia Ofisi iliyokuwa relini, ambayo haikuwa na mazingira rafiki kiutendaji na kupelekea kuomba kupata Ofisi itakayowezesha Wananchi kupata huduma katika mazingira rafiki" alisema Ndugu Zuberi ambaye ni Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mtakuja wakati akisoma risala kwa Mgeni Rasmi ambaye ni Meya wa Manispaa ya Ilala.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mhe. Charles Kuyeko akizindua rasmi jengo la Ofisi ya Mtaa wa Mtakuja katika Kata ya Vingunguti










Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi