WAZIRI JAFO ATOA SIKU 45 KWA UONGOZI WA SOKO LA SAMAKI FERI KUKARABATI MIUNDOMBINU

Na: Anna Chiganga Utouh news

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo ametoa siku 45, kwa mamlaka husika katika soko la Samaki Feri lililopo katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kufanya Ukarabati wa miundombinu ya soko hilo ambayo imeharibika na kusababisha mazingira magumu ya kazi kwa Wafanyabiashara wa eneo hilo.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo katika ziara aliyoifanya katika soko hilo ambapo amekagua miundombinu mbalimbali ikiwepo barabara ya soko hilo, meza, choo pamoja na maji ambapo amesema Wafanyabiashara hao wanalipa kodi hivyo ni haki yao kuwepo kwa miundombinu rafiki na salama kwao.

"Nitakuja hapa baada ya siku 45, kuona mazingira yamerekebishwa na nitoe maelekezo kwa Injinia ahakikishe barabara hii imetengenezwa na tarehe 23, mwezi Julai nitakuja hapa kuangalia utekelezaji wa ukarabati wa mazingira haya kwani hili ni soko kubwa ambalo linakuza uchumi wao na wa Nchi kwa ujumla" Amesema Jafo.

Aidha, amesema anataka waakina  Mama li waliokuwa wakifanya biashara katika eneo hilo na kutolewa warudishwe na kuwataka akina Mamantilie hao kufuata sheria na kuwa mlinzi kwa kila mmoja kuhakikisha wanaofanya biashara za madawa ya kulevya wanabainishwa.

" Nataka wakina mama waliokuwa wanafanyabiashara ya chakula hapa Sokoni warudishwe na kuendelea na kazi zao ili kuwarahisishia wafanyabiashara kupata chakula kwa urahisi na kuwataka Mamantilie hao kuhakikisha kila mmoja anakuwa mlinzi wa mwenzake ili kubaini wanaopita na kutumia madawa ya kulevya"Amesema

Waziri Jafo amesema kuwa ameuzunishwa na uongozi unavyofanya kazi katika eneo hilo kwani Wananchi wanapata shida kutokana na miundombinu mibovu.

Pia amemtaka Meneja wa soko hilo kuhakikisha wanatenga sehemu za akina Mama Lishe ili waendelee kufanya biashara kutokana na kutolewa maeneo hayo kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya Kulevya.

"Meneja wa Soko hakikisha mnatenga sehemu maalumu ya  kina Mama Lishe ili waweze kuendeleza biashara yao na wanaofanya shughuli zao hapa waweze kuwa na uhakika wa kupata chakula sehemu salama na rahisi kwao" Amesema Waziri Jafo.

Pia ameutaka Uongozi kuhakikisha wanatatua changamoto zilizopo katika soko hilo kwani ni sehemu kubwa ambayo Wananchi wanaofanya biashara zao na kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao, pamoja na kuinua uchumi wa Nchi na si kusubiri Waziri afike kutoa maelekezo.

Kwa Upande wake Meneja wa Soko la Samaki Feri Bwana Mkuu Hanje amesema kuna Jengo ambalo lipo katika soko hilo na kwamba linadaiwa kuwa ni la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambapo hawakusanyi Kodi kutoka katika jengo hilo hivyo wanashindwa kulikarabati kutokana na kuwa liko chini ya Manispaa.

Amesema watahakikisha yote aliyoyasema Mhe. Waziri yanafanyiwa kazi kikamilifu na kuondoa kero na changamoto zilizopo.

Nao Wafanyabiashara wa soko hilo wamekiri kuwepo kwa changamoto hizo na wamemshukuru Mhe. Waziri kwa kufika na kuwasaidia ili changamoto hizo ziweze kutatuliwa na kuweza kufanya kazi Katika mazingira rafiki na salaama ili kukuza uchumi wao binafsi na Taifa kwa ujumla.






Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi