HABARI PICHA: MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJIRI MANISPAA YA ILALA KWENYE JUMA HILI

Na: Hashim Jumbe
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akitoa maelekezo wakati wa zoezi la usafi uliofanyika Jumamosi kwenye fukwe za Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema akishiriki zoezi la usafi kwa kuzoa taka kwenye eneo la fukwe za Bahari ya Hindi karibu na Hospitali ya Aga Khan ikiwa ni moja ya shughuli zilizofanyika kwenye wiki ya mazingira

Baadhi ya Watumishi wa Manispaa ya Ilala walioshiriki kwenye kilele cha siku ya Mazingira Duniani eneo la fukwe za Bahari ya Hindi ambapo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu alizindua ukuta unaokinga kingo za bahari zisimomonyoke

Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Bibi Elizabeth Thomas wa kwanza kushoto akipokea Kikombe cha ushindi wa jumla kwenye mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa mwaka 2018
Mkuu wa Idara ya Mazingira Manispaa ya Ilala Bwana Abdon Mapunda akimkabidhi cheti cha shukrani Afisa Uhusiano Manispaa ya Ilala Bibi Tabu Shaibu. Cheti hicho ni kuthamini mchango na ushiriki katika Mazingira

Mratibu wa Kampeni ya Bint makini, Mwamvuli wangu stara Bibi Tabu Shaibu aliyepo upande wa kushoto akipokea mchango wa ujenzi wa choo cha Mtoto wa Kike kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Manispaa ya Ilala Bibi. Esther Masomhe


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi