Na: Hashim Jumbe
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, hatimaye timu ya Wilaya ya Ilala imefanikiwa kubeba ubingwa wa jumla kwenye mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa mwaka 2019.
Ubingwa huo umepatikana kufuatia timu ya Ilala kuibuka washindi wa kwanza kwenye mchezo wa mpira wa miguu wavulana, mpira wa miguu wasichana, mpira wa miguu kwa wanafunzi wenye ulemavu-viziwi, mpira wa pete, mpira wa mikono wavulana, mpira wa mikono wasichana, riadha na fani za ndani kwa upande wa ngoma.
Aidha, mashindano hayo, yaliyodumu kwa siku Tano (5) yamefungwa rasmi jioni ya leo katika viwanja vya Uhuru Jijini Dar es Salaam na Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Hamis Lissu, na kuundwa kwa timu ya Mkoa wa Dar es Salaam inayotarajia kuingia kambini siku ya Jumamosi kwa maandalizi ya siku Tano (5) kwaajili ya mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Taifa yanayotarajiwa kuanza kufanyika Mkoani Mtwara mwishoni mwa mwezi huu.
Ikumbukwe kuwa, Ubingwa walioupata Ilala mwaka huu wa 2019 unaifanya Ilala iingie kwenye historia ya mashindano hayo ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kubeba Ubingwa wa jumla mara Nne (4) mfululizo.

Tags:
HABARI