Na: Mariam Hassan
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Ndugu Jumanne K Shauri amewataka wafanyabiashara katika Halmashauri hiyo kulipa kodi kwa wakati.Akiongea na waandishi wa habari katika kikao alichofanya nao katika ukumbi wa arnatouglou kuhusu ukusanyaji wa mapato kwenye Halmashauri hiyo kufikia billioni 56.
Ndugu Jumanne .K. Shauri amesema ukusanyaj wa mapato katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala unatakiwa uwe billion 56 lakini hadi kufikia mwezi mei 2019 fedha zilizokusanywa n billion 52 ambayo ni 92% ikiwa ni upungufu wa billioni 4 kukamalisha ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri hiyo.
''Katika Halmashauri yetu ya Manispaa ya Ilala kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 tulipanga tukusanye billioni 56 lakini kutokana na changamoto kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wachache kutokulipa kodi kwa wakati mapato hayo hadi kufika mei 2019 tumekuwa na upungufu wa billioni 4.''Alisema Jumanne Shauri
Aidha Mkurugenzi Shauri amesema amewapa siku 14 wafanyabiashara wote ambao hawajalipa kodi katika Halmashauri hiyo kwani adhabu kali itachukuliwa na watalipishwa faini ifikapo tarehe 1 mwezi 7.
''Nawapa siku 14 kwa wale wafanyabiashara wote ambao hawajalipa mapato ya Halmashauri ifikapo tarehe 1 mwezi wa 7 watachukiliwa hatua kali na pia watalipishwa faini.''Alisema Ndugu Shauri
Akielezea faida zinazotokana na ulipaji wa kodi za Halmashauri amesema tumeboresha miundombinu mbalimbali kama vile kujenga shule mpya za msingi na za sekondari pamoja na maboresho ya upatikanaj wa huduma bora za afya na pia tumetoa mikopo kwa vikundi vya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu kwa mwezi Aprili, 2019 tumeweza kutoa Shilingi 1.7 Bilioni