ZIARA YA KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA KATIKA UKAGUZI WA MIRADI

Na: Mariam Hassan
Kamati  ya  Fedha na Utawala  Manispaa ya Ilala, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Omary  Kumbilamoto  jana imefanya ziara ya ukagua wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwa kipindi cha robo ya nne ya Aprili hadi Juni katika sekta ya Elimu, Masoko na pia kutembelea ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mzinga.

Katika ziara hiyo walitembelea Soko jipya la Kisutu na kujionea namna ujenzi unavyoendelea, lakini pia walitembelea Shule ya Sekondari Kinyamwezi kukagua ujenzi wa maboma sita yanayoendelea kujengwa shuleni hapo na Shule ya Sekondari Kitunda inayojengewa maboma manne na kuhitimisha ziara hiyo kwa kukagua ujenzi wa ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mzinga.

Ujenzi wa Mradi  wa  soko  la Kisutu  kukamilika kwake kutagharimu Shilingi Bilioni 2.15 na mpaka   mpaka  sasa  umefikia  hatua  nzuri
Wajumbe wa Kamati ya Fedha  na Utawala Manispaa ya Ilala wakipokea maelezo kutoka  kwa  mkandarasi wa  Ujenzi  wa  soko  la Kisutu na  kumuonyesha hatua  aliyofikia. 

Mwenyekiti  wa  Kamati  ya  Fedha  na Utawala  Mh.Omari Kumbilamoto akipokea maelekezo ya ujenzi wa maboma sita ya shule ya sekondari  Kinyamwezi kutoka  kwa mkuu wa shule hiyo Bi.Sifa Mwakaluka.  



Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi