Na: Hashim Jumbe
Waswahili husema 'nyota njema huonekana asubuhi', na ndivyo ilivyoanza kuonekana kwa Manispaa ya Ilala wakati huu wa maonesho ya 26 ya Wakulima na Wafugaji maarufu kama 'Nane Nane' yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. J.K Nyerere Mkoani Morogoro, ambapo kwa Kanda ya Mashariki yakishirikisha Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Morogoro yenyewe.
Maonesho hayo kwa mwaka huu wa 2019 yanabeba kauli mbiu isemayo 'Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi' huku lengo la maonesho hayo likiwa ni kuwatambua na kuwaenzi wadau wakuu wa Sekta ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maliasili kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu.
Aidha, maonesho ya Nane Nane hutoa fursa kwa Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na Wadau mbalimbali kuweza kuona na kujifunza mbinu na teknolojia sahihi za uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili na bidhaa nyinginezo.
Ikiwa ni siku ya pili tangu kuzinduliwa kwa maonesho hayo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema pamoja na Viongozi wengine wa Manispaa ya Ilala, wameridhishwa na kupongeza jitihada zilizofanyika ndani ya Manispaa ya Ilala ikiwa ni pamoja na kuwawezesha Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na wadau wengine kupata nafasi ya kujifunza kupitia maonesho hayo.