Na: ESHA MNYANGA
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Omary Kumbilamoto, ametembelea na kukagua mradi wa mazingira wa uboreshaji na
upendezeshaji Mji uliopo uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dad
es salaam kwa lengo la kujiandaa na mapokezi ya wageni wa Jumuiya ya nchi za
kusini mwa Afrika (SADC) wanaotarajiwa
kuwasili hivi punde.
Katika
ziara hiyo, Mh Kumbilamoto ameiagiza Idara ya Mazingira na Usafishaji Manispaa ya
Ilala kuendeleza zoezi la usafishaji wa mazingira katika Manispaa hiyo kila baada ya mwezi mmoja.
Aidha,
Mhe. Kumbilamoto ametoa wito kwa Watanzania pamoja na Wajasiriamali wote
kutumia fursa hiyo ya ujio wa wageni kwa kufanya biashara zao ndogondogo
ikiwemo uuzaji wa bidhaa za asili ya kitanzania ili waweze kujikwamua kiuchumi
na kufikia malengo yao vile vile waweze kuitangaza Tanzania.
Kwa
upande wake Mkuu wa Idara ya Mazingira na Usafishaji Manispaa ya Ilala Ndg.
Abdon Mapunda, ameeleza jitihada walizozifanya katika utekelezaji wa mradi huo
kwani walianza zoezi la usafi pamoja na upakaji rangi vigingi vya barabarani
mwanzoni mwa Julai 2019 na hatimaye kufikia leo wamemkabidhi Meya Mh. Omary Kumbilamoto ili aweze kukagua utendaji wao wa kazi.
Kutoka
na kuridhishwa na utendaji kazi mzuri uliofanywa na Idara hiyo, ndipo Mstahiki
Meya Mh. Omari Kumbilamoto ameweza kutoa zawadi ya mbuzi wawili kwa idara ya
mazingira.
muonekano mpya wa barabara ya Nyerere baada ya kufanyiwa uboreshaji |