Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh Mwita Waitara ameipongeza
shule ya Sekondari Juhudi iliyopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,
kwakufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu kwa kuzipiku
shule nyingi kongwe hapa jijini kwa kupata daraja la kwanza hadi la tatu tu. Naibu waziri ameyasema hayo alipoitembelea
shule hiyo Agosit 9 mwaka huu katika ziara yake ya ukaguzi wa mradi wa Makitaba
shuleni hapo.
Akikagua ujenzi wa maktaba shuleni hapo, Mh Waitara
amepokea na taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kutoka kwa Makamu Mkuu wa shule
hiyo Mwalimu Koka Delvini ambaye amethibibitisha kwamba mradi huo uPo katika
hatua za mwisho kukamilika na mwishoni mwa mwezi huu utakuwa tayari na wataweza
kukabidhi ili Serikali iwezeshe upatikanaji wa vifaa vingine kama vitabu, viti
na meza kwa maktaba hiyo.
Sambamba na ukaguzi wa mradi huo Mh. Naibu Waziri
aliweza kuzungumza na wanafunzi kwakuwasisitizia wajitume katika masomo yao
kwani wao ndiyo Taifa la kesho na waunge mkono juhudi za Mh Rais Dk John P.
Magufuli za kuleta Sera ya Elimu bure toka kidato cha kwanza mpaka cha nne kwani
kufaulu kwao ndiyo furaha ya Rais wetu pia wazazi wao wanawategemea.
Wakati Mh Waziri akizungumza na Wanafunzi hao
aliwaelezea kwamba “baada ya kumaliza kuongea nanyi hapa nataka niandaliwe
Darasa la kidato cha nne ili niweze kuwafundisha somo la hisabati’ hivyo baada
ya hotuba fupi ya waziri aliingia darasani na kufundisha somo hilo jambo ambalo
walimu na wanafunzi walifurahia sana kwa kitendo cha waziri kufundisha shuleni
hapo, akizungumzia hatua hiyo ya Mhe. Naibu Waziri mwanafunzi Salehe Juma
alisema “tumefarijika sana kufundishwa na Waziri”
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh.Mwita Waitara akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Juhudi |