WAFANYABIASHARA SOKO LA KISUTU WAJITOKEZA KUCHANGIA DAMU


Na Hucky Hamis, Judith Damasi na Rafiki Ally
Wafanyabiashara soko la Kisutu Manispaa ya Ilala Jijini Dar-es-saalam wamejitokeza kwa wingi katika zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na zahanati ya KISUTU SPECIALIZED POLY CLINIC leo tarehe 15 Agosti 2019. Zoezi hilo limefanyika kwaajili ya kuokoa maisha ya majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro mnamo  tarehe 10 Agosti2019 na pia kuwasaidia wagonjwa wengine wenye uhitaji wa damu.

Akizungumza na wandishi wa habari Ndug. Zuberi Luhono ambaye ni Mwenyekiti wa Soko la Kisutu amesema kuwa “baada ya uhamasishaji  huo wafanyabiashara 58 wakiwemo 32 kutoka  soko la Matunda na 26 kutoka soko la Mkunguni wameonekana kuguswa na wito huo hivyo kuamua kujisajili kwaajili ya zoezi hilo la uchangiaji damu”

Aidha Dkt.Majidi Mfaume kutoka hospitali ya mkoa Amana, amesema kuwa “uhitaji  wa damu  ni mkubwa kulingana na mahitaji ya wagonjwa kwani kwa siku hutumia zaidi ya uniti 50 za damu  lakini mchango wanaoupata kwa wachangiaji ni uniti 20 tu ambazo huwa hazitoshelezi kwa mahitaji ya wagonjwa” hivyo amewataka wananchi wazidi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo ili kuokoa maisha ya  wengine.

Hata hivyo mmoja wa wafanya biashara wa Soko hilo Bw.Alex  Matei  ameonekana  kuguswa na zoezi hilo la uchangiaji damu hivyo kutoa wito kwa wafanyabiashara wenzake wajitolee kwa wingi katika zoezi hilo ili kuokoa maisha ya wengine.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi