Na, Esha, Rafiki, Hucky, Judith, Mariam, Ruth, Sabina na Lulanga.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Omary
Kumbilamoto amekabidhi vifaa vya choo (masinki 10) pamoja na bati 20 katika
shule ya sekondari kinyamwezi iliyoko kata ya pugu Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam.
Makabidhiano hayo niutekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati
kamati ya fedha ilopofanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo. Katika
shule ya Sekondari Pugu Kinyamwezi Kamati ilibaini kuwepo kwa changamoto
mbalimbali ikiwemo uchakavu na ubovu shuleni hapo
Akisoma risala kwa Mgeni
Mh. Omary Kumbilamoto, Mkuu wa Shule hiyo Bi.Sifa Mwaruka amesema
wanakabiliana na changamoto ukilinganisha na mafanikio wanayopata, changamoto
hizo ni uchache wa matundu ya vyoo vya wanafunzi na walimu kwani walimu wanatumia vyoo vinne ambavyo wanaume
wanatumia viwili na wanawake viwili, na idadi ya walimu nikubwa ukilinganisha
na idadi ya vyoo, uchache wa viti vya
wanafunzi na walimu pamoja na meza za kusomea
, ukosefu wa uzio hali ambayo ina sababisha
wanafunzi kutoroka kihorela na migogoro ya mipaka katika eneo la shule
kwani wananchi hujenga katika maeneo ya shule .
Kufuatia tukio hilo Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala
amezipokea changamoto hizo na kuahidi
kuzifanyia kazi. Aidha Mstahiki Meya ametoa wito kwa wanafunzi kuzingatia
maudhui yaliyopo katika wimbo wa shule ili kuepuka vishawishi ili wafikie malengo yao na kusisitiza usafi.
Akitoa neno la shukran mwanafunzi wa shule hiyo Peace
Mustic wa kidato cha nne amesema shule
inakabiliwa na changamoto nyingi ila wanaamini kuwa zitashughulikiwa, nakuahidi
kutunza vifaa hivyo na kumuomba Mstahiki Meya
kuwa Mgeni Rasmi katika mahafali
yao yatakayofanyika mwezi wa kumi mwaka
huu wa 2019.
Tags:
HABARI