Na: Hashim Jumbe
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) leo limetangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la Saba, uliofanyika nchini kote tarehe 10 na 11 Septemba, 2019, ambapo Manispaa ya Ilala imeweza kushika nafasi ya 5 kati ya 186 kwa Halmashauri zote zilizofanya mtihani huo.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Charles Msonde amesema "kwa ujumla matokeo yamepanda kwa ufaulu wa ongezeko la 3.78%"
Aidha, kwa upande wa Manispaa ya Ilala ufaulu umeongezeka kutoka 95.59% ya mwaka 2018 hadi 96.77% kwa mwaka huu wa 2019, ikiwa ni ongezeko la 1.18%, ingawaje Manispaa ya Ilala imerudi nyuma kwa nafasi moja kutoka nafasi ya Nne (4) kwa mwaka 2018 hadi nafasi ya Tano (5) kwa mwaka 2019.
Katika matokeo hayo, Jumla ya Wanafunzi 13,698 wa Manispaa ya Ilala kutoka Shule 113 walifanya mtihani huo na waliofaulu ni 13,256 sawa na 96.77% huku Wanafunzi 442 sawa na 3.33% wakishindwa kufanya vizuri mtihani huo.
Kwa matokeo hayo, inaonesha pia Wasichana wa Manispaa ya Ilala wameweza kupandisha viwango vya ufaulu, kwani idadi ya waliofanya mtihani kwa mwaka 2019 ilikuwa ni 7,061 na waliofaulu ni 6,830 sawa na 96.16% ukilinganisha na mwaka 2018, waliofanya mtihani walikuwa 6,851 na waliofaulu walikuwaa 6,495 sawa na 94.80%.
Kwa upande wa Wavulana na wenyewe wameweza kupandisha ufaulu, kwani waliofanya Mtihani mwaka 2019 walikuwa 6,637 na waliofaulu ni 6,426 sawa na 97.87% ikiwa ni tofauti na mwaka jana, kwani Wavulana walikuwa 6,217 na waliofaulu ni 5,997 sawa na 96.46

Tags:
HABARI