Na: Hashim Jumbe
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Bw. Jumanne Shauri, leo ametembelea vituo vya uandikishaji wa wapiga kura na kujionea namna zoezi hilo linavyoendelea katika vituo mbalimbali vya Manispaa ya Ilala.
Aidha, Mkurugenzi Shauri amepongeza mazingira ya vituo hivyo, kwani yamekuwa ni rafiki kwa wanaofika kujiandikisha "hadi sasa changamoto tulizokuwa nazo kwenye zoezi hili la uandikishaji ni mvua iliyonyesha siku mbili za mwanzoni, lakini kwa upande wa vifaa vya uandikishaji tunavyo vya kutosha na makarani wana uweledi wa kutosha wa zoezi hili, hivyo ukifika vituoni ni kama sekunde 30 unakuwa umeshaandikishwa"
Lakini pamoja na ukaguzi wa vituo vya kupigia kura, lakini Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala hajaridhishwa na muitikio wa Wananchi wanaoendelea kujitokeza kwenye zoezi hilo la uandikishaji "bado namba ya Wananchi wanaojitokeza hairidhishi, tumepanga kuandikisha 100% ya maoteo yetu au izidi hapo ili kila Mwananchi mwenye sifa aweze kutumia haki yake ya kikatiba"
Wakati huo huo, Mkurugenzi Shauri ameongeza nguvu ya kuhamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uandikishaji, kwa kuamua kuingia mitaani na kutoa matangazo "leo Mkuu wetu wa Wilaya ameingia mitaani na yeye kutoa matangazo ya uhamasishaji Wananchi wakajiandikishe, na mimi nimeongoza Watendaji wangu kupita mtaa kwa mtaa kutoa matangazo"
Mkurugenzi Shauri ameongeza "naamini kwa siku hizi za mwisho wa jumaa uandikishaji kwa Manispaa ya Ilala utaongezeka kwani Wananchi wengi waliokuwa wakikosa muda wa kujiandikisha kutokana na kutingwa na majukumu ya kazi"
Sambamba na hayo, Mkurugenzi Shauri aliendelea kuwaasa Wananchi kutokubali kurubuniwa na Watu wasiowatakia mema "tumesikia kuna Watu wanapita kuwarubuni kuwa msijitokeze kujiandikisha, niseme Watu hao hawawatakii mema, nendeni mkajiandikishe mpate sifa ya kuchagua Viongozi mnaowataka, kwani maendeleo yanaanza kupangwa ngazi ya mtaa"