UHAMASISHAJI WA SURUA RUBELLA KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA.

Na Mariam Hassan

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Jumanne Shauri amewasisitiza
watendaji wa Kata pamoja na Wenyeviti wa serikali za mitaa kuwahamasisha wananchi
wenye watoto kuanzia miezi 9 hadi miaka mitano (5) kuwapeleka watoto kwenye chanjo
ya Surua Rubella inayotolewa katika Kata 36 pamoja na Mitaa 159 ya Manispaa ya Ilala.

Mkurugenzi aliyaeleza hayo katika kikao cha uhamasishaji pamoja na kuwasisitiza
Watendaji wa kata na wenyeviti wa mitaa kutoa ushirikiano kwa watoa huduma ya
chanjo walioko katika maeneo yao.



Pichani ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Jumanne K. Shauri akiwa
anazungumza na Watendaji pamoja na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa.


Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Dr.Emily Lihawa amesema hadi
zoezi hilo kukamilika Halmashauri inategemea kutoa chanjo ya Surua Rubella kwa
watoto 191,502 pamoja na walengwa wa polio ya Sindano 113,797 zitakazotolewa katka
vituo 182 vikiwa na watoa huduma 910. Vituo vinavyohusika na zoezi hilo ni Zahanati,
Vituo vya Afya, Hospitali na Ofisi zote za Serikali za Mtaa.

Mganga Mkuu wa Halmashauri Dr Emily Lihawa akitoa taarifa ya namna chanjo
zitakavyotolewa katika maeneo yote ya Halmashauri.


Pichani ni wajumbe wa kikao wakiwa ni Watendaji wa Kata pamoja na Wenyeviti wa
Mitaa


Watendaji wa Kata pamoja na Wenyeviti wa Mitaa wakiwa katika kikao

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi