Na: Hashim Jumbe
Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Manispaa ya Ilala, leo tarehe 28 Aprili, 2020 imefanya ziara yake ya kawaida kukagua Miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kipindi cha Robo ya Tatu ya Januari-Machi, 2020, huku Wajumbe wa Kati hiyo wakichukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona, kwa kuvaa Barakoa na tahadhari nyengine.
Aidha, Kamati hiyo inayosimamia Miradi katika Sekta za Afya, Elimu, Kilimo, Uvuvi na Ufugaji ilitembelea Shule mpya ya Sekondari ya Minazi Mirefu ambayo ujenzi wake unakaribia kukamilika, miradi mingine waliyotembelea ni Machinjio ya Kisasa ya Vingunguti, Ujenzi wa Vyumba Vinne vya Madarasa Shule ya Sekondari Mchanganyiko na Ujenzi wa Soko la Kisasa la Kisutu.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Abdulkarim S. Masamaki akiongea wakati wa majumuisho ya ziara hiyo alisema "Nimeridhishwa na hali ya Miradi inavyokwenda, na ninawaomba Halmashauri muendelee kuisimamia miradi hii ikamilike kwa wakati uliowekwa, na miradi ambayo imetolewa mapendekezo na Wajumbe, nayo muifanyie kazi"