Na: Amanzi Kimonjo
“Tunatekeleza agizo la Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. SAMIA SULUHU HASANI, katoa maelekezo kwamba pamoja tupo katika maombolezo lakini kazi za kuwatumikia wananchi ziendelee” alisema Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam, Mhe. Omary Kumbilamoto akiwa katika ziara ya ukaguzi wa ujezi wa shule mpya ya Kipunguni na Bwawani, alipotembelea tarehe 31 Machi, 2021
Ujenzi wa Shule ya Sekondari Kipunguni madarasa kumi yamejengwa na ujenzi upo 90% kumalizika ikiwa ni sehemu ya mipango ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kuhakikisha haki hii ya msingi kwa watoto inamaana elimu inatolewa kwa kila mtoto wa kata ya Kipunguni katika hili ni sehemu moja wapo na hatua kubwa katika kuondoa adha ya watoto wa kata ya kipunguni ambao walikosa majengo ya shule kwa sekondari sasa yapo tayari.
Mstahiki Meya akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Jiji la Dar es salaam Ndg Tabu Shaibu alitoa pongezi kwa Mkurugenzi wa
Jiji la Dar es salaam kwa miradi hii mikubwa inayoendelea na kuleta
maendeleo kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam na nchi nzima.
Mstahiki Meya akiwa kata ya Kipunguni alisisitiza ushirikiano katika uongozi hasa viongozi wa wa chama, pamoja viongozi wa mtaa kwa maana wenyeviti wa mtaa kushirikiana sanjari na Diwani.
Aidha ,Mstahiki Meya alitembelea pia mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya Bwawani na kutoa pongezi kwa Halmashauri kwa ujenzi huo
Kutoka Kushoto : Diwani wa Kata ya Kiwalani Mh. Musa Kafana, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mh. Omary Kumbilamoto, Afisa Elimu Sekondari Ndg. Mussa Ali, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu