Waziri Mkuu Majaliwa atembelea machinjio ya Vingunguti

 Na: Judith Damas

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa  amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kuhakikisha kuwa hadi kufikia Juni 30 , 2021 Machinjio ya  kisasa ya Vingunguti ianze kufanya kazi ili kuhakikisha tunapata nyama yenye thamani zaidi ambayo itauzwa hadi nje ya Nchi ya Tanzania.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Vingunguti katika ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya mradi wa Machinjio ya kisasa ya Vingunguti leo Mie17,2021 Waziri Mkuu ameeleza kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia 95 ikiwemo ujenzi wa visima vya kuchuja maji taka, vyumba vya kuhifadhia nyama pamoja na chumba cha kuchomea mizoga hivyo kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kuhakikisha kuwa Marekebisho madogomadogo yaliyosalia  kukamilika katika machinjio hayo  ili yaanze kufanya kazi rasmi.

Sambamba na hilo Waziri Mkuu amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kuhakikisha wanaziba mifereji ya maji  na kujenga mifereji maaulum yakupitisha maji ili kuzuia maji kutiririka na kuharibu miundombinu ya na mikazi ya  watu.

 

 


" Niwaagize Jiji kuhakikisha kuwa wanajenga mifereji maalumu ya kupeleka maji mtoni na hivyo kwenye hizo asilimia tano(5)zilizobaki  mjenge mifereji hiyo ili kuhakikisha maji yanaenda mtoni  na sio kwenye mikazi  ya watu". Amesema Waziri Mkuu.

Aidha Waziri Mkuu amemwelekeza Mwenyekiti wa wajasiriamali kwenye machinjio hayo kuhakikisha   wananashirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ili kuweza kumaliza tofauti zao na kuzungumza lugha moja.

 

 


"Ningetamani sana kama tungeweza kuanza kutumia machinjio haya ya Kisasa hata leo  lakini pia mwenyekiti wenu ameniambia ni vyema tukamilishe kwanza ujenzi huu, ila na mimi ningewaomba mshirikiane na Halmashauri ya Jiji ili muweze kuwa kitu kimoja ili kuweza kufanikisha jambo hili na pia muda mwingine mnaweza kutafuta ngo'mbe na kuja kuchinja huku ili kuwafanya wachinjaji kuzoea na mara baada ya kuanza kutumia machinjio haya ya kisasa ya Vingunguti kazi ziwe zinaenda kwa uharaka zaidi"

Vilevile, Waziri Mkuu  amemuhakikishia Mbunge wa Jimbo la segerea kuwa suala la ajira kwa vijana waliopo maeneo ya machinjio hayo amelipokea moja kwa moja na anamuachia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam atakapotangaza ajira aanze na vijana hao wanaofanya kazi katika machinjio ya zamani kwani wanauzoefu mkubwa  zaidi.

 


 Kwa upande wake Naibu waziri wa Ardhi Mhe.Anjelina Mabula amewapongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ambao wamebuni mradi huo wa kimkakati wenye mafanikio chanya kwa wananchi na hivyo kumuahidi Waziri Mkuu kusimamia mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati.

"Sisi kama Wizara ambao tunasimamia kile ambacho unaelekeza na tutawasimamia National Housing kufanya ile kazi ambayo utakua unaelekeza kwani mradi huu wa kimkakati utakapokamilika vijana watapata ajira  na kukuza uchumi pia." Amesema Mhe. Mabula.

Akitoa taarifa ya mradi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam  Ndug.Jumanne Shauri ameeleza kuwa machinjio ya vingunguti yamefikia asilimia 95 za utekelezaji na yamegharimu takribani Shilingi Bilioni 12.49 mpaka kukamilika kwake na hivyo amemuahidi Waziri Mkuu kuwa hadi kufikia Juni 30, 2021 mradi huo utaanza kutumika rasmi ambapo utawanufaisha wananchi wengi na pato la Halmashauri litaongezeka.

 


 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi