DC Ilala azindua zoezi la Upimaji Afya bure kwa Wakazi wa Wilaya ya Ilala

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Ngw'ilabuzu Ludigija leo Juni 11 amezindua zoezi la Upimaji Afya Bure ambalo litafanyika kwa muda wa siku mbili kaanzia Leo tarehe 11 hadi 12 Juni 2022 katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam ambapo Wakazi wakazi  wa Wilaya ya Ilala  watapata Fursa ya kupima magonjwa Bure Chini ya madaktari bingwa na wabobezi.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam  Mheshimiwa Ludigija  amesema lengo la Kampeni ni kuwafikia wananchi wengi zaidi wa Wilaya ya Ilala kwani ni fursa pekee kwa wananchi wasio na bima za afya, watoto yatima pamoja  na wananchi wote wasio na uwezo wataweza kuhudumiwa bure lengo likiwa nikuhakikisha afya za Watanzania zinakua imara zaidi.

 


Hata hivyo mheshimiwa Ludigija amesema" katika zoezi hili madaktari bingwa kutoka Hospital mbalimbali watahudumu zikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Ocean Road, Taasisi ya mifupa MOI, Hospital ya Taifa Muhimbili, Agakhan, Chama Cha madaktari, Saifee, Hospital binafsi na Hospital za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pia  miongoni mwa huduma zitakazotolewa ni upimaji magonjwa yasiyoambukizwa ikiwemo Kisukari, Shinikizo la Damu, Saratani na magonjwa mengineyo hivyo tujitokeze kwa wingi kutumia fursa hii adhimu na ya kipekee ya kuimarisha afya zetu."

 


Sambamba na hilo "Serikali ya Awamu ya tano ya Mheshimiwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anataka wananchi wawe na afya bora kwani ukiwa na afya bora utaweza kufanya kazi kwabidii na ndio maana Rais wetu amekua akiboresha huduma za afya na ujenzi wa vituo vya afya vya karibu na makazi ya wananchi ili kuweza kupata huduma kwa ukaribu zaidi hivyo niwaombe mzingatie mlo sahihi na pia muhakikishe elimu mtakayoipata hapa mnaemda kuwa mabalozi kwa wengine ambao hawajafika waweze kufika kucheki afya zao kwani afya ni mtaji."Ameeleza Mheshimiwa Ludigija.

 


Aidha Mheshimiwa Ludigija amewashukuru na kuwapongeza Wadau waliofanikisha zoezi Hilo ikiwemo  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na  Clouds Media Group chini ya Mkurugenzi Joseph Kusaga, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Ocean Road, Hospitali ya Taifa Muhimbili, MOI, AghaKhan, PCMC, TMH, Chama Cha Madaktari, Red Cross, hospital za Halmashauri ya Jiji la Dar as Salaam, kampuni ya simu ya Vodacom pamoja na wadau mbalimbali waliojitokeza kufanikisha zoezi hili hivyo kuwaasa wananchi wajijengee utaratibu wakucheki afya zao mara kwa mara.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi