RC Chalamila aridhishwa na mapokezi ya awali ya wanafunzi Jiji la DSM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila ameridhishwa na mapokezi kwa wanafunzi wa awali na darasa la kwanza kwa shule za msingi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam .


Hayo ameyaeleza Leo Januari 8, 2024 wakati wa ziara ya kukagua mapokezi ya wanafunzi wa darasa la awali na darasa la kwanza ikiwa ni siku ya kwanza kwa mwaka mpya wa masomo 2024.

Shule alizozitembelea ni pamoja na shule ya Msingi Muhimbili ambayo Hadi Leo imepokea wanafunzi wapya wa darasa la kwanza 157, ambapo wavulana ni 84 na wasichana 73 na Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa waliojiandikisha Hadi Leo ni wanafunzi 101, wavulana wakiwa 43 na wasichana 58.

Akizungumza na walimu na wazazi wa shule hizo baada ya ukaguzi Mhe. Chalamila amesema “Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga miundombinu bora ya elimu ili wanafunzi wote wapate elimu iliyo bora. Pia nawaonya wakuu wa shule zote kutoingia tamaa ya kuchangisha michango kwa wanafunzi iliyo kinyume na sheria kwa manufaa yake binafsi , atakayebainika sheria kali itakuchuliwa dhidi yao. Vilevile wazazi hakikisheni watoto wanaotakiwa kuwa shule wanaripoti bila kujalisha wana ulemavu au hawana sare za shule."


Sambamba na hilo RC Chalamila amesema "Mapokezi ni mazuri kwa shule zote na hii ni siku na wiki ya kwanza , hivyo tutarudi tena baada ya miezi mitatu hasa kwa shule za sekondari Ili kuona kama kuna haja ya kufanya uchaguzi wa pili (second selection) kwa wanafunzi ambao hawakubahatika kupata shule.


Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Ilala  Mhe. Edward Mpogolo amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuja kuangalia mapokezi ya awali ya uandikishaji wa awali wa wanafunzi na kumuhakikishia kutatua changamoto zote za elimu zinazokabili shule za Wilaya ya Ilala.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi