Kamati ya Ngozi Halmashauri ya Jiji la DSM yajipanga kuboresha zao la ngozi kuwa la kibiashara

Kamati ya ya Ngozi ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, yajipanga kuboresha zao la ngozi kuwa la Kibiashara zaidi, hayo yamebainishwa leo tarehe 26 Februari, 2024 na Wajumbe wa Kamati ya Ngozi wakati wa Ziara ya mafunzo ya uchakataji wa ngozi. Katika kiwanda cha Farwa International Limited.


Wakiwa kwenye ziara hiyo Wajumbe waliweza kutembelea eneo la uchakataji wa ngozi lililopo majumba sita ambapo wajumbe waliweza kuangalia uchakati wa ngozi pamoja na kujifunza namna zao la ngozi linavyoandaliwa hadi kufikishwa sokoni.


Akiongea wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Ngozi Mhe. Moza Mwano ameeleza kuwa “Ngozi ni zao la ziada linalotokana na mifugo ambalo hutumika kama malighafi muhimu katika viwanda vya ngozi na huingiza fedha nyingi za kigeni kwani kutokana na maelezo ya mchakataji inakadiriwa kuwa ngozi zote huuzwa nje hususani Nchini Nigeria na hutumika kama chakula hivyo kwa mazingira haya inabidi Kuboresha uzalishaji, ukusanyaji na usindikaji wa ngozi kwa ajili ya soko la ndani na nje ili kuongeza kipato katika Halmshauri yetu kutokana na zao la ngozi."


Awali akitoa maelekezo ya namna ya uchakataji wa ngozi, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda Hicho Bw. Hemed Yusuph Salum ameeleza kuwa kwa upande wao hununua ngozi kavu kutoka maneno mbali mbali ya Nchi, hivyo wao huongezea ubora kwa kupulizia dawa ya kuua wadudu na kuuza nje ya nchi.


Aidha, kutokana na umuhimu wa zao la ngozi kibiashara, Kamati imependekeza Halmashauri itenge eneo nzuri la uchakataji wa ngozi pamoja na shughuli nyingine zinazozlishwa na kutokana na zao la ngozi kwani zao hilo litakua chachu ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi