Wajumbe wa Halmashauri Kuu wapitisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama katika Halmashauri ya Jiji la DSM

Katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Februari 9, 2024 Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala imepokea Taarifa ya Utekelezaji wa miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia Januari-Juni 2023.


Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Arnatouglou Jijini DSM na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala, Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala, Mkuu wa Wilaya wa hiyo, Wajumbe wa Halmashauri Kuu Wilaya ya Ilala pamoja na Watumishi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.


Akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala Ndg. Alhaji Said Sidde amesema “Niwapongeze Wajumbe wa Halmashauri Kuu kwa kupokea na kupitisha Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pia nipende kuipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutekeleza Ilani ya Chama kwani wameweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuboresha huduma za wananchi. Niwaombe viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha mnatekeleza yale yote tuliyowaelekeza wakati wa ziara yetu na pia muhakikishe miradi yote inatekelezwa kwa wakati uliopangwa."


Akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Edward Mpogolo ameeleza kuwa “Katika kutekeleza Ilani, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Idara zake zikiwemo Idara ya Elimu, Idara ya Afya, Idara ya Maendeleo ya Jamii pamoja na Idara ya Maliasili na Mazingira ambapo katika Idara ya Elimu Msingi na Sekondari, Halmashauri ya Jiji la DSM imeendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022-2022/2023 jumla ya Tsh 15,100,339,616/=. Pia kwa upande wa kuboresha miundombinu ya Elimu za kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022-2022/2023 miradi hiyo ina thamani ya Tsh 25,755,408,582.5 utekelezaji wa wa miradi hii umetokana na fedha kutoka Gharama za mpango wa Elimu bila malipo, Serikali Kuu, Mapato ya Ndani ya Halmashauri na wafadhili, SEQUIP na BARRICK. Pia miundombinu ya Afya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kipindi cha miaka mitatu imepokea kiasi cha Tsh 11,346,768,015, zikiwa ni za ukarabati wa miundombinu chakavu, Ujenzi wa vituo vipya vya Afya na ununuzi wa vifaa tiba. Kwa upande wa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imefanya uhamasishaji na kutoa mikopo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, Halmashauri imeweza kutoa kiasi cha Tsh 27,359,233,000 kwa vikundi 1963. Pia tumejitahidi kusimamia usafi wa mazingira kwa kusimamia wakandarasi wa uzoaji taka na vikundi vya uzoaji taka na kufanya mazingira safi zaidi."


Sambamba na hilo Mhe. Mpogolo ameendelea kusema “Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya Wilaya ya Ilala, pia Halmashauri ya Jiji tupo tayari kupokea maelekezo yote na kuyatekeleza kwa maslahi ya wananchi wa Wilaya wetu."


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi