Kuelekea Kilele cha maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano, Jiji la DSM laandaa mashindano ya michezo na ngoma

Katika kuelekea Sherehe za Kilele Cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo Aprili 20, 2024 imeandaa mashindano ya michezo na ngoma yenye lengo la kushajaisha na kupamba shamrashamra za Maadhimisho hayo.


Akiongea wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yaliyofanyika kweye Viwanja vya Magereza - Ukonga, Afisa Michezo, Utamaduni na Sanaa Ally Lugendo amesema mashindano hayo ni muhimu kwa kudumisha Muungano lakini pia ni sehemu ya kukuza michezo na kuibua vipaji.


Michezo iliyochezwa ni Mpira wa Miguu kwa wavulana na wasichana, mpira wa wavu, pamoja na Mashindano ya ngoma.












Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi