Dar yang'ara Maonesho ya Sabasaba 2024

Mkoa wa Dar es Salaam umefanikiwa kuchukua ushindi wa kwanza, wa pili na watatu katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 48 (Sabasaba) katika Kipengele cha Mamlaka za Serikali za Mitaa .

Mshindi wa Kwanza ni Manispaa ya Kinondoni, Wa pili Manispaa ya Temeke na Wa tatu Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Pichani Mratibu wa Maonesho ya Sabasaba wa Sekretarieti ya Mkoa wa Dar es Salaam Bw Thabit Massa akiwa pamoja na Wawakilishi wa Wakurugenzi wa Kinondoni, Temeke na Jiji baada ya Kupokea Ngao na Vyeti vya Ushindi

Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 29.06.24 yalifungwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ally Mwinyi tarehe 13.07.2024.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi