Wanafunzi 145 wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Kinyamwezi wamefanya ziara ya mafunzo katika Makumbusho ya Kale yaliyopo Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo lengo la ziara hiyo ya siku moja (1) lilikuwa ni kujifunza kwa vitendo somo la Historia pamoja na kujua Tamaduni mbalimbali za kale.
Kwa upande wake Mwl. Donald Madandi ambye ni mwalimu wa somo la Historia ameeleza kuwa wanafunzi hao wamefanya ziara hiyo kwa lengo la kupanua mawazo yao namna ya kutumia historia kama nyenzo ya kujifunzia juu ya mambo ya kale.
“Mimi kama Mwalimu wa Historia nimeandaa ziara hii ya kimasomo kwaajili ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa kidato cha kwanza katika somo la historia ili waweze kulielewa vizuri kwani kupitia ziara hii naamini wanafunzi hawa watapata kufahamu mambo mbalimbali ya Kihistoria ikiwa pamoja na kujifunza mifumo ya maisha waliokua wakiishi hapo kale kama vile Ujima hivyo tofauti na ziara hii kuwasaidia katika somo la Historia pia itawasaidia wanafunzi kuelewa mila na desturi mbalimbali za jamii na namna ya kuishi vizuri katika jamii zao”. Amesema Mwl. Madandi.
Akiongea kwa niaba ya Wanafunzi wenzake Hesbon Nashon ameeleza kuwa “Ziara hii ya kimasomo imetusaidia vizuri kujua mambo mbalimbali ya kihistoria tunayojifunza darasani lakini pia mbali na hapo tumeweza kufahamu mila na desturi za zamani na maisha ya kale yalivyokua hivyo tunaahidi tutaishi kulingana na mila na desturi zetu pamoja na kuheshimu tamaduni zetu”.