"Tuchochee Uchumi kwa kuwekeza Nchini" - Afisa Tarafa Ukonga

Wakazi wa Jiji la DSM wamepewa Wito wa kuwekeza nchini kwani Serikali ya awamu ya sita imeweka mazingira rafiki, kwani kwa kufanya hivyo kutachochea maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Afisa Tarafa Ukonga Ndg. Kheri William (aliyesimama) akiongea na wafanyakazi na wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Hoteli ya L21 Executive Hotel

Wito huo umetolewa na Afisa Tarafa Ukonga, Kheri William, alipokuwa Mgeni Rasmi akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, wakati akifungua L21 Executive Hotel ya muwekezaji Mzawa iliyoko Kata ya Kitunda, Jijini Dar-es-salaam iliyogarimu zaidi ya million 300 iliyo mita chache kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Afisa Tarafa Ukonga Ndg. Kheri William akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Hoteli ya L21 Executive

Akiongea wakati wa ufunguzi huo, Ndg. William amesema "Uwekezaji huu utaongeza ajira, kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza ukusanyaji wa Kodi mbalimbali za Serikali.


Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mama yetu shupavu SSH imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji na ukusanyaji wa kodi rafiki isiyotumia nguvu
"


Naye Diwani wa Kata ya Kitunda Mhe. Victor Vedasto alitoa pongezi kwa wamiliki wa Hoteli ya L21 Executive kwani kwa uwezekezaji huo wametengeneza fursa za ajira na kuongeza ukusanyaji wa Kodi.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi