Na Judith Damas na Mariam Hassan
Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Ilala Bw. Mussa Ally amewahimiza walimu wakuu kutimiza wajibu na kuwa na ushirikiano baina yao wenyewe na viongozi wao wa kata ili kuboresha ufaulu, Ameyasema hayo leo tarehe 7/1/2021 katika kikao kazi cha kufanya maandalizi rasmi ya ufunguzi wa Shule kilichofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Tambaza.
Afisa Elimu Sekondari Bw. Mussa Ally
Baadhi ya walimu wakuu wa shule za sekondari za Manispaa ya Ilala waliofika katika kikao kazi hicho wakisikiliza kwa makini
Vilevile Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ndug. Jumanne Shauri ameongezea kuwa kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa pamoja na madawati hivyo Halmashauri yatoa zaidi ya billioni nne kwa ujenzi wa madarasa na ukarabati wa madawati ili kuhakikisha ifikapo february 28 wanafunzi wote wa sekondari Wilaya ya Ilala wanaingia darasani bila changamoto yoyote.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ndg. Jumanne Shauri akihotubia
Pia, amewasisitiza Walimu wakuu wote, Maafisa Elimu Kata, Madiwani na Watendaji wa Kata kufanya kazi kwa kushirikiana kwa amani na uelewano baina yao.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Mh. Omari Kumbilamoto amewaahidi Wakuu wa Shule pamoja na Maafisa Elimu Kata amewaahidi kuwapa ushirikiano kwa lolote litakalotokea atahakikisha atapambana nalo ili idara ya Elimu Sekondari kufanya vizuri.
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Omari Kumbilamoto
Mwalimu Mkuu Shule ya Sekondari Tambaza Bw. Husein Zuberi Mavumba ametoa shukrani kwa Mkurugenzi na Mstahiki Meya kwa kuwaahidi watafanya kazi kwa bidii na kasi kubwa sana.