Na David Langa.
Diwani wa kata ya Kipawa katika halmashauri ya Manispaa ya Ilala jiji Dar es salaam Mh. Bonna Kalua amewaomba wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao ndiyo wahanga wakubwa wanaoathirika kwa kukosa damu.
Mh. Kalua aliyasema hayo katika tamasha la kuchangisha damu katika viwanja vya Stakishari vilivyopo ukonga katika kata ya Kipawa ambapo zaidi ya chupa 300 zilichangwa na watu mbali mbali waliofika siku hiyo wengi wao wakiwa wanamichezo toka vikundi mbali mbali vya michezo jijini Dar es salaam.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa ambaye alisema "Tunaweza kununua dawa na vifaa vyote vya kimatibabu lakini kamwe hatuwezi kununua damu". Mh. Silaa aliyasema hayo kutokana na kuwa duniani kote hakuna nchi yenye kiwanda cha kutengeneza damu na hivyo ni wajibu wa wananchi wenye afya kujitolea damu ili kuweza kuokoa maisha ya wenzao.

Mmoja wa watu waliojitokeza kuchangia damu Mwl. Juma Orenda wa shule ya Sekondari Mvuti akijitolea ikiwa ni kuunga mkono juhudi za kuokoa maisha ya mama na mtoto |
Mganga mkuu wa Manispaa ya Ilala Dr. Willy Sangu (mwenye track nyeupe)akimuongoza mgeni rasmi Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa kuingia katika viwanja vya Stakishari |
Mtumishi kutoka mpango wa Taifa wa damu salama ndg Towo akitoa maelezo kwa mgeni rasmi namna wanavyoendesha shughuli zao. katikati ni diwani wa kata ya Kipawa Mh. Bonna Kalua. (picha na David Langa) |